Jinsi ya Kutengeneza Pesa Mtandaoni

Hello, Habari za mda huu, Leo tunaenda kujifunza ni namna gani tunaweza kujiingizia kipato mtandaoni, aidha kipato cha pembeni tofauti na kazi kuu (Part Time) au kipato kikuu (Full time Job). Mfumo wa utengenezaji Pesa uko hivi, kwa wale wanao wekeza pesa hua wanatumia juhudi ndogo na mda mchache kufikia malengo, ingawa kwa wale wanao jiwekeza wao kama wao hua wanatumia juhudi nyingi na mda mwingi kufikia malengo. Kwa kifupi wenye mitaji hela huwafanyia kazi lakini kwawasio namtaji wao huifanyia kazi hela

Iwe ni mtandaoni au iwe ni kazi za nje, Hamna hela rahisi wala ya haraka, watu wengi wamekua wakidaganyika hata kutapeliwa na kupotezewa mda wao kwa kushirikishwa katika njia zisizo na ukweli mfano Kutengeneza pesa kwa kuangalia video, sijui kujibu maswali na nyingine nyingi. Sisemi yakua njia halali zinazolipa kwa kufanya hivyo vitu hazipo, ni vile hata zilizopo zinamalipo madogo sana ambayo hayato kuongezea chochote katika maisha yako

Kwa kusema hayo leo nitaenda kuwafundisha Njia kadhaa ambazo nina uhakika nazo ya kua zinafanya kazi vizuri hata kwenye soko letu la Afrika mashariki na pia ukiwekeza juhudi lazima utayaona matunda

1.Uuzaji wa Bidhaa Mtandaoni– Ikiwa tayari unabidhaa yako, lakini unahangaika kuitafutia wateja basi mtandaoni kuna soko kubwa mno la bidhaa yako. Katika mitandao ya kijamii kama tiktok, facebook, instagram na mengineyo humo unaweza kufungua account special kwa ajili ya bidhaa au duka lako baada ya hapo itakubidi uanze kutengeneza Content nzuri na zenye kuvutia ili uweze kunasa wateja kwa urahisi, ukishabatika kupata wateja wawili watatu, faida utakayo kua umeipata itakubidi uiwekeze kwenye matangazo ya mtandaoni, haya yatakusaidia kuvuna wateja wengi kwa urahisi. Kwa wanaohitaji msaada jinsi ya kutengeneza matangazo yanayoleta wateja unaweza kututafuta tukusaidie. Whatsapp Us

2.Blogging (Mwanabloggia)– Kumekua na maneno mengi watu wakidai ya kua blogging imekufa hasa hiki kipindi ambacho watu wanapenda kutumia mitandao ya kijamii tu. Wenda unajiuliza Blogging ni nini? Kukurahisishia kuelewa, hili jarida unalolisoma nalo ni Blog, hivyo Blogging inahusisha kuandika nakala zako nakuzichapisha mtandaoni, ambapo itakubidi uwe na tovuti. Katika Blogging unaweza kutengeneza pesa kwa kuweka matangazo katika blog yako, kuuza huduma zako pia unaweza uza bidhaa ya mtu mwingine na ukapokea commission kutoka kwake hivyo inakubidi blog yako iwe na watembeleaji wengi ili uweze kupata wateja hao. Kama utahitaji kufahamu zaidi juu ya blogging usisite kututafuta kwa elimu zaidi Whatsapp Us

3.Youtube & Tiktok (Content Creation)- Tukianza na Tiktok, utengenezaji wa pesa moja kwa moja bado haujafika Barani Africa, ingawa wataalamu wanasema unaweza pambana na kufungua account ya marekani, lakini fahamu ya kua unaweza pata utata mkubwa katika kuitoa pesa hiyo. kwa njia nyingine unaweza kupata pesa kupitia tiktok Live kwa kupewa Gifts na mashabiki zako pia ukiwa creator mzuri, unaweza tafutwa na makampuni ili uwatangazie biashara zao, Kwenye upande wa Youtube utahitajika upate Subscribers 1000 na Watazamaji waliozitama video zako kwa ujumla ikamilishe masaa 4000. Kuanzia hapo utaweza ku apply ili uweze kutengeneza pesa youtube. Kumbuka youtube inahitaji Original Content (Content ulizotengeneza wewe mwenyewe) Kwa Elimu zaidi Whatsapp Us

4.Biashara ya Sarafu za Kidigitali (CryptoCurrency)- Hapa nitawafundisha jambo tofauti kabisa na Trading. Kumekuwa na ongezeko kubwa la vijana wanaopambana kutengeneza pesa mtandaoni, ingawa wengi wao wanapopata pesa hizo wanashindwa kuzipokea kwenye wallet zao wanazozipenda kama M-Pesa, TigoPesa, Airtel Money na nyinginezo. Kwa hiyo, kama wewe ni wakala au unamtaji wa angalau Laki Tano na zaidi, unaweza kuwa daraja. Kwa mfano, kama mtu ana USDT 200 na ameshindwa kuzitoa kwenye app kama bitcoin, Payoneer, PayPal, Web Money au nyinginezo, yeye atakutumia hio USDT 200 kwenye akaunti yako kwenye app hiyo, halafu wewe utamtumia pesa yake kwa njia ya M-Pesa lakini kwa rate ya chini, mfano USDT 1 ni sawa na Tzs 2700 wewe utaiuza Tzs 2500. Hivyo, kwa kila USDT moja, utapata faida ya Tzs 200. Mfano, akiwa na USDT 200, utapata faida ya Tzs 40,000. Pia unaweza kusubiri dhamani ya dola ipande ili uweze kutoa pesa yako kwa faida kubwa zaidi.

🤩 Tuambie Kwenye Comment Tuongeze Kuielezea njia Gani ambayo ungependa Kuifahamu zaidi 🤩

Reviews

74 %

User Score

47 ratings
Rate This

Sharing

Leave your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 Comments